Akili Unde kutwaa ajira za watu zaidi ya 4,000 benki ya DBS

 

Benki kubwa ya nchini Singapore imesema inatarajia kupunguza wafanyakazi zaidi ya 4,000 miaka mitatu ijayo, wakati huu ambapo kazi nyingi za binadamu zikifanywa na Akili Unde (AI).

Benki hiyo ya DBS imesema kazi hizo zitakazochukuliwa na Akili Unde ni zile za muda mfupi na za mikataba katika kipindi cha miaka michache ijayo.

Watumishi wenye mikataba ya kudumu hawatodhurika na zoezi la kupunguza wafanyakazi.

Mtedaji Mkuu wa Benki hiyo anayeondoka Piyush Gupta amesema kuwa DBS inatarajia kutengeneza ajira 1,000 zinazohusiana na Akili Unde.

Taarifa hii inaifanya benki ya DBS kuwa benki ya kwanza kubwa kutoa taarifa za jinsi Akili Unde itakavyobadili utendaji wa benki hiyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni