Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza vyombo vya dola kuwakamata waliohusika na mauwaji ya Dk Isack Daniel Athuman yaliyofanyika mkoani Kata ya Nyamongo Tarime vijijini mkoani Mara .
Waziri Ummy ametoa agizo hilo kupitia akaunti yake katika mtandao wa twita ambapo ameonesha masikitiko yake kutokana na tukio hilo.
Aliandika “Very sad kupoteza mtaalamu wetu wa afya. Ninalaani vikali tukio hili. Pole kwa familia na watumishi wote wa sekya ya Afya Tarime na nchini kwa ujumla! May his soul rest in peace”
Nakusisitiza kuwa “Tunaamini vyombo vya dola vitafanikisha kupatikana kwa wahusika waliofanya kitendo hiki”
Wengine ambao walionesha kuguswa na tukio hilo ni Dk Elisha Osati ni rais wa chama cha madaktari Tanzania MAT ambaye aliandika “Haikubaliki.Dr Isack ni mmoja wa Madaktari 1000 tuliopewa na Rais Magufuli katika maadhimisho ya siku ya Madaktari 2020”.
“Isack alikuwa tayari kuwahudumia wananchi vijijini hivi utamwambia Dr gani akafanyekazi Tarime,Tunaitaka mamlaka iwakamate wahusika bila kumung'unya maneno” ameandika Osati
Festo Ngadaya ni daktari na mratibu wa elimu ya afya mtandaoni aliweka picha wakiwa makaburini baada ya kumzika marehemu na kuandika waraka mrefu “Pumzika mwanangu, mapanga na nondo ulizopigwa Tarime na kumwaga damu yako havitaenda bure”
Hakusita kutoa ya moyoni na kuandika “Inanikumbusha kipindi kile daktari alichelewa kwenye ajali namna uongozi wa wilaya mpaka mkoa ulicharuka, leo kauwawa kitu pekee wametoa ni tangazo la TANZIA tena wakificha kuwa kauwawa”
Miongoni mwa taarifa zinazosambaa mtandaoni ni pamoja na tangazo la tanzia lilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime likieleza masikitiko ya kumpoteza mtumishi huyo wa afya.
Marehemu Dk Isack Daniel Athuman Sima alikuwa ni Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Nyangoto kilichopo Kata ya Nyamongo, Tarime Vijijini.
Dk Sima, anadaiwa kuuwawa kwa kukatwakatwa Mapanga na Watu Wasiojulikana wakati akitoka kituo chake cha kazi usiku wa Mei 3,2023 akirejea nyumbani.
0 Maoni