Ujumbe wa anko HK!Siyo kila mtu unamuambia mambo yako

 

Mbunge wa Nzega na aliyewahi kuwa Waziri wa mali asili na Utalii Dk Hamis Kigwangalla kwenye ukurasa wake mtandao wa Facebook leo May 6 ameandika 

Kuwa makini sana na yule mtu mmoja unayemuamini sana kiasi kwamba unafunguka mambo yako kirahisi sana mbele yake, huyo ndiye chanzo cha kuanguka kwako. Jifunze kunyamaza. Ni kazi, lakini jifunze. Utanishukuru siku moja. 

Hizi ni kanuni za kuwafundisha watu wema na wazuri, ambao wamekuwa wakichezewa sana na watu washenzi! 

Hebu zingatia haya:

1. Hata siku moja usije ukamuambia mtu yeyote yule mipango yako. Watu huwa wana tabia za kuhujumu mipango ya wengine. 

2. Hata siku moja usije ukajikuta unafunguka kiasi cha kumueleza mtu yeyote yule madhaifu/mapungufu yako. Eti unamuamini sana kiasi kwamba unataka akujue vizuri ili mwende sawa. Hususan pisi umeielewa fulani hivi! Trust me, atatumia madhaifu/mapungufu yako kukumaliza. 😩

3. Usije ukarogwa ukamhadithia mtu siku ulipowahi kufeli huko nyuma, atakusikiliza vizuri sana na atakuchukulia wewe kama mtu wa kufeli siku zote. Hatokuja kukuamini na kukupa mchongo hata siku moja. 

4. Ukiwa na jambo lako kubwa linakuja mbele, usipende kuwaambia watu. Fanya kwanza, ‘kimya kimya’ kisha waoneshe matokeo tu. Vinginevyo, watakukwamisha kabla hata haujaanza. 

5. Usimwage siri zako kwa mtu yeyote yule! Narudia. ‘Mtu yeyote yule.’

6. Usitegemee chochote kile kutoka kwa mtu yeyote yule. Siku zote jiandae kuangushwa na watu. Watu humu duniani siyo waaminifu; wengi ni wabinafsi, wanafiki na wasaliti! Jiamini mwenyewe tu. Cover all ground, be on top of your game. 

7. Usije ukamwambia mtu yeyote yule unapopatia hela zako. Akiujua mrija wako basi kuwa na hakika ataenda kuukata, kuutoboa ama kuuhamishia kwake, kama asipouwekea sumu! 😩

8. Usijitambulishe kwa kutumia nguvu sana juu ya uwezo wako kifedha ama kimamlaka, ama title yako ya kitaaluma ama kicheo. Hujui mimi ni ‘Dr.’? Hujui mimi ni ‘Mhe.’ Zingatia tu kuwa noti huwa haipigi kelele, kelele huwa ni za masile sile! 

Chapisha Maoni

0 Maoni