Rais Samia atoa maagizo kuanza mchakato wa Katiba mpya

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuagiza msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi kuitisha kikao maalumu cha Baraza la vyama vya siasa.

TAZAMA VIDEO

Rais Samia ametoa maagizo hayo leo Mei 6, 2023 Ikulu ya Chamwino Dodoma  wakati akiongoza Kikao cha Viongozi mbalimbali wa Serikali kinachohusu kuanza kwa Mchakato wa Katiba mpya.


Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus imesema Rais Samia amesisitiza  lengo la kuitisha mkutano huo ni kuwashirikisha wadau katika kutathmini utekekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi nchini.



Mbali na mchakato wa katiba mpya masuala mengine yanayotarajiwa ni pamoja na marekebisho ya sheria mbalimbali.

Chapisha Maoni

0 Maoni