Jeshi la polisi lataka wenye ukweli kifo cha mwanafunzi UDOM kujitokeza


Baada ya siku moja kupita toka Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kutoa  taarifa kuhusu kifo chenye utata cha mwanafunzi Nusura Hassan Abdallah.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania SACP David Misime amesema jeshi hilo limebaini kuwepo kwa taarifa katika mitandao ya kijamii ikihusisha kifo hicho na ajali ya gari iliyotokea jijini Dodoma ikimuhusisha Naibu waziri Tamisemi Dk Festo Dugange.



Katika taarifa SACP Misime imesema jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro baada ya kuwepo kwa taarifa hizo imeanza kufanya uchunguzi kwa watu mbalimbali ikiwemo hospitalini alipotibiwa binti huyo na kushirikisha ofisi ya mkemia mkuu, DPP na wadau wengine wa haki jinai.




Pia jeshi hilo limetaka mtu yeyote ambaye ana taarifa sahihi na zenye ukweli asisite kuzitoa ili kuharakisha uchunguzi.SOMA ZAIDI



Chapisha Maoni

0 Maoni