Pande mbili zinazokizana katika kilichokuwa chama tawala
Kenya cha Jubilee, zimekimbilia kwa Msajili wa Vyama vya Siasa Anne Nderitu ili
amalize mgogoro wao wa kuwania madaraka, ambapo kila upande unataka kuwatimua kwenye
chama wenzao.
Upande unaoongozwa na rais mstaafu Uhuru Kenyatta, umeiandikia
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, wakitaka mbunge wa kuchaguliwa Sabina
Chege aliyeanzisha uasi na kuteuliwa kuwa kiongozi wa chama pamoja na mbunge
Kanini Kega kufutwa uanachama.
Kenyatta anawatuhumu wabunge hao wawili kwa kukiuka Katiba
ya chama kwa kuunga mkono sera za Rais William Ruto za chama cha UDA.
Kama hiyo haitoshi, wabunge hao wawili pia wamekuwa
wakituhumiwa kwa kuanzisha uasi dhidi ya viongozi wa chama cha Jubilee, jambo ambalo
ni ukiukaji mkubwa wa Katiba ya chama.
0 Maoni