Aliyekuwa Rais wa Marekani, Joe Biden, ameanza
kupatiwa matibabu ya mionzi (radiation therapy) kama sehemu ya tiba yake dhidi
ya saratani ya tezi dume, msemaji wake amethibitisha.
Kwa mujibu wa msemaji huyo, Biden mwenye umri wa
miaka 82 pia anapatiwa matibabu ya homoni, ingawa hakufafanua zaidi kuhusu
hatua hiyo ya matibabu.
Taarifa kutoka kwa chanzo kilichoelezwa na shirika
la habari la NBC News zinaeleza kuwa matibabu ya mionzi yanatarajiwa kuchukua
kipindi cha wiki tano, hali inayochukuliwa kama hatua mpya katika safari yake
ya kiafya.
Biden aliondoka madarakani mwezi Januari akiwa Rais
mzee zaidi kuwahi kuhudumu katika historia ya Marekani, na hali ya afya yake
iliibua maswali mengi wakati wa muhula wake wa kwanza.
Maswali hayo yalimfanya hatimaye kuamua kujiondoa katika
kinyang’anyiro cha kuwania urais kwa muhula wa pili, akiwa tayari ameanza
kampeni za kuchukua tena nafasi hiyo.

0 Maoni