Afisa wa Polisi auawa kwa mshale akilinda ikulu ya Nairobi

 

Afisa mmoja wa polisi aliyekuwa akilinda moja ya lango la Ikulu ya Rais jijini Nairobi nchini Kenya amefariki dunia baada ya kupigwa mshale, maafisa wa usalama wamethibitisha.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, tukio hilo lilitokea Jumatatu asubuhi wakati mwanamume mwenye umri wa miaka 56, akiwa amejihami kwa upinde na mishale, alipoelekea kwa maafisa wa polisi waliokuwa wakilinda lango hilo la Ikulu.

Mwanaume huyo alipoamriwa ajisalimishe, alikaidi na badala yake akampiga PC Ramadhan Matanka mshale kifuani, upande wa mbavu, taarifa ya BBC imeeleza.

Afisa huyo alikimbizwa hospitalini kwa matibabu ya dharura lakini alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Shambulio hilo limeibua maswali kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa mapungufu katika ulinzi wa Ikulu, eneo ambalo linahesabiwa kuwa miongoni mwa yanayolindwa kwa ulinzi mkali zaidi nchini Kenya.

Chapisha Maoni

0 Maoni