WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa leo Oktoba 14, 2025 ameshiriki katika Ibada ya kumuombea
Baba wa Taifa Hayati Mwalimu. Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika
Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Francisko wa Asizi, Mwanjelwa Mkoani
Mbeya.
Makamu wa
Rais Dkt. Philip Isdor Mpango pia ameshiriki katika ibada hiyo.
Ibada
hiyo imeongozwa na Akofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mbeya Mhashamu Gervas
Nyaisonga



0 Maoni