Rais Trump atia saini agizo la kuiwekea vikwazo Mahakama ya ICC

 

Rais Donald Trump ametia saini agizo la kuiwekea vikwazo Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), akiituhumu kuwa “sihalali na kufafanya vitendo vinavyokiuka sheria kwa Marekani na mshirika wake wa karibu Israel.”

Vikwazo hivyo ni vya kifedha na kunyiwa viza kwa watumishi na familia zao waliohusika katika kuwachunguza raia wa Marekani na washirika wake.

Rais Trump ametia saini hatua hizo wakati ambapo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akitembelea Washington.

Novemba mwaka jana, ICC ilitoa hati ya kukamatwa Netanyahu kwa tuhuma za uhalifu wa kivita huko Gaza, tuhuma ambazo Israel imezikanusha. ICC pia ilitoa hati ta kukamatwa kamanda wa Hamas.

Chapisha Maoni

0 Maoni