Ulimwengu wa sayansi na teknolojia unasonga
kwa kasi ya ajabu. Mataifa makubwa duniani yanawekeza kwenye ubunifu, utafiti
wa kisayansi, na teknolojia za kisasa.
Teknolojia kama akili unde, kilimo cha kisasa
na tiba za kibunifu zaidi zinabadilisha maisha katika mataifa makubwa duniani.
Karne ya akili unde [AI], roketi zinavuka
anga, kuna uvumbuzi na gunduzi nyingi katika teknolojia mpya kwa kasi ambayo
dunia haijawahi kushuhudia.
Mataifa makubwa yanawekeza, yanashirikiana, na
yanapasha habari za sayansi kwa umma wao kwa kasi.
Lakini upande mwingine wa dunia, ndani ya
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika [SADC], bado kuna pengo kubwa katika
mawasiliano ya sayansi.
Watafiti wanagundua, Serikali zinafanya
miradi, taasisi zinavumbua, lakini taarifa 'hazitembei' kwa kasi inayohitajika.
Bado haziwafikii vema wananchi wake, hazijengi
uelewa na hazifanyi sayansi kuwa sehemu ya maisha ya kila siku.
Ndani ya SADC, bado kuna pengo kubwa kati ya
maendeleo ya ki-sayansi na jinsi ambavyo taarifa hizo zinavyowafikia wananchi.
"Kwa sababu nchi nyingi za SADC bado
hazina mkakati wa mawasiliano katika masuala ya sayansi,".
Yameelezwa hayo na Mkurugenzi Mkuu wa
Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika, Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu
(DSTI), Afrika Kusini Mwampei Chaba.
Ni wakati alipokuwa akifungua mdahalo wa siku moja wa waandishi wa masuala ya sayansi kutoka nchi 18 wanachama wa SADC.
Amesema kutokana na pengo lililopo katika
upashanaji habari kuhusu maendeleo ya sayansi katika nchi hizo, ndiyo maana
DSTI iliona vema kuwaleta pamoja waandishi wa habari na kufanya mdahalo huo.
Ni katika mkutano wa kimataifa wa waandishi wa
habari za masuala ya sayansi [WCSJ2025] unaofanyika Pretoria nchini Afrika
Kusini.
Akifungua mjadala huo, aliweka wazi changamoto
kubwa wanazokutana nazo waandishi wa sayansi katika ukanda huu.
“Nchi nyingi katika SADC bado hazina mkakati
wa ushirikiano katika mawasiliano kuhusu sayansi. Hiyo ndiyo sababu upashanaji
habari za sayansi unakumbwa na changamoto nyingi.”
Ameongeza "Ukosefu wa mkakati huo
unawafanya waandishi wengi kukosa ushirikiano wanaohitaji kutoka kwa Serikali
zao.
"Mnashindwa kuwa karibu na watafiti,
mnakosa mazingira rafiki ya kupata habari, pamoja na fursa za ufadhili au
mwaliko kwenye matukio muhimu yanayohusu sayansi na uvumbuzi.
Amesisitiza "Kwa hivyo, katika nchi yako
na unataka kupata ushirikiano kutoka Serikali [kuandika kuhusu habari fulani
inayohusu sayansi] au unataka watambue kazi yako.
"Unataka kufadhiliwa kwa baadhi ya kazi
zako. Unataka kualikwa kwenye matukio [kwa wengi wenu], itakuwa ngumu kwa kuwa
hawana mkakati wa ushirikiano kuhusu hilo," amesema.
"Mkirudi nchini mwenu kafuatilieni hili
kwa undani, nendeni mkaulize wizara [zinazohusika na masuala ya] sayansi,
wizara za mawasiliano [iwapo] wameandaa mkakati?.
Hii ni mara ya kwanza kwa Bara la Afrika kuwa
mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa waandishi wa habari za sayansi, afya,
mazingira na mambo mengine yanayohusiana na hayo.
Mdahalo huo kwa ajili ya waandishi wa habari kutoka SADC ulilenga kuwaleta pamoja kujadiliana namna gani watasukuma mbele masuala ya sayansi ndani ya nchi zao kwa upashanaji habari.
"Hii ni warsha ya mafunzo yenye umuhimu
mkubwa kwetu. wazo hili lilikuja kwetu mwaka 2022 tulipoandaa Mkutano wa
Sayansi Duniani (World Science Forum).
"..,, ambao ulikuwa wa kwanza kuandaliwa
barani Afrika. Kwa hivyo, tulitengeneza historia mwaka 2022 kwa kuandaa mkutano
wa Sayansi Duniani barani Afrika.
"Kisha tukaamua kuwa kuleta fursa kama
hii barani Afrika bila waandishi, waandishi wa sayansi kuwa kwenye chumba,
kungekuwa kupoteza.
Ameongeza "Tunawezaje kuwasilisha kile
tunachofanya katika mkutano, kama idara, kama serikali barani Afrika, kama
taasisi zinazofanya utafiti, ikiwa hatuna uandishi wa sayansi kwenye chumba?
"Pia tuligundua kuwa waandishi wa sayansi
bado hawana uwezo wa kutosha kuhusiana na uandishi na kuandika makala za
sayansi.
"Hivyo basi, tuliona hitaji la kuunda
ushirikiano. Na Stellenbosch alishirikiana nasi kwa kiwango kikubwa.
Amesema walianza kupanga warsha ya mafunzo,
yenye vipengele vingi, ambayo itasaidia kujenga uwezo wa waandishi wa habari
katika kuwasilisha kazi tunazofanya kwa ufanisi zaidi.
"UNESCO ilifadhili baadhi ya wajumbe
mwaka 2022, na imeendelea kuwa mshirika wetu tangu wakati huo.
"Sekretari ya SADC pia imekuwa mshirika
wetu, na tunashukuru sana michango waliyotoa kwa waandishi wa SADC kuungana
nasi.
"Chama cha Waandishi wa Sayansi wa Afrika
Kusini (SASJA) pia kimeungana nasi, na sisi pia tuko kwenye mshirika mkubwa
katika mkutano mwingine wa kihistoria," amebainisha.
Amesema mkutano wa WCSJ2025 walioandaa mwaka
huu unatengeneza historia mpya nyingine na walitaka kuwa sehemu ya historia
hiyo.
Amesema Afrika Kusini waliunda mkakati wa
mawasiliano na ushirikiano katika masuala ya sayansi tangu mwaka 2015 na kwamba
walichelewa mno kuunda.
"Taasisi yetu ilianzishwa Juni 2004,
hivyo karibu miaka 11 baadaye, tu wakati huo tu tulikuwa na mkakati wa
ushirikiano wa sayansi unaotekelezwa kwa sasa, na mchakato wa ukaguzi upo.
Amebainisha "Mwaka huu SADC ilishiriki
katika G20. Tulikuwa Rais wa G20 na GSTI ilipanga kile kinachoitwa Wiki ya
Utafiti na Ubunifu [Research and Innovation Week].
"Pia tulipitisha hati maalumu inayoitwa
Azimio la Ushirikiano wa Sayansi wa G20 (G20 Science Engagement Resolutions).
"Hati hiyo inahimiza nchi za G20 kuweka
sayansi kati-kati ya jamii inahimiza kuongeza ufahamu katika jamii zetu kuhusu
thamani ya sayansi, na kuwasilisha sayansi kwa njia jamii zinaweza kuelewa.
"Kwa nini tunapaswa kufanya hivyo? Ni kwa
nini hii ni muhimu? Sayansi haifadhiliwi vya kutosha, na hili ni changamoto
katika jamii nzima.
Amesisitiza "Ikiwa thamani ya sayansi
haifahamiki, ikiwa athari ya sayansi haijulikani kwa serikali zetu, jamii zetu,
wafadhili wetu na wachangiaji.
"Basi mpango wa kufafanua ni ninyi
walioko hapa. Ninyi ndio midomo yetu. Ninyi ndio mabalozi wetu wa kuwasilisha
sayansi kwa jamii.
"Mara sayansi itakapofahamika, mara thamani ya sayansi itakapothibitishwa kwenye hatua za vitendo, kwenye jamii, kwenye vijiji.
"Basi mna nafasi nzuri ya kupata ufadhili
kutoka Serikalini, ufadhili kutoka kwa wafadhili na kadhalika.
"Kwa hivyo, jukumu lenu ni muhimu sana,
na tunategemea ninyi kusaidia kuunganisha pengo," amesema na kuongeza.
"Napenda kuwahimiza kwamba katika wiki
hii, mchukue fursa ya warsha nyingi zinazofanyika kuhamasisha sayansi,”
alisema.
"Matumizi ya data, sita-sita kusema
kwamba sayansi inapaswa kuwa kati-kati ya jamii, elimu, viwanda, ili kuendesha
maendeleo kwa ujumla.”
"Na haiwezi kuwa katikati ikiwa ninyi
hufahami jinsi ya kuwasilisha sayansi. Nami naamini hatuhitaji kuwa wanasayansi
ili kuelewa sayansi.
"Sayansi inapaswa kufafanuliwa kwa mtu wa
miaka 85 na mtoto wa miaka 5. Bila kutumia maneno magumu.
Amesisitiza "Ikiwa mtu hawezi kueleza,
ikiwa mwanasayansi unayemhoji hawezi kueleza sayansi yao kwa njia unayoielewa,
basi hawafanyi kazi nzuri.
"Na pia unapaswa kuwa na uwezo wa
kuhimiza wanasayansi kuzungumza na kuwasilisha sayansi kwa njia kila mtu
anaweza kuelewa.
Amehoji "Je, unajua waandishi mashuhuri
wa sayansi barani Afrika? Kwa nini haingewezekana iwe wewe?
"Kwa nini haingewezekana iwe wewe?”
aliuliza, akiwahimiza washiriki kuwa wao wenyewe wanaweza kuwa waandishi
mashuhuri wa sayansi Barani Afrika.
“Kuna waandishi wa sayansi mashuhuri duniani kote, lakini sio barani Afrika. Afrika inahitaji sayansi kwa maendeleo zaidi kuliko kanda nyingine yoyote duniani.
"Hivyo basi, tufanye lengo letu kuwa na
waandishi mashuhuri wa sayansi katika jamii zetu, nchi zetu, ndani ya SADC na
barani kote.
Amesisitiza "Vinginevyo, mbona mko hapa?
Kwa nini mko hapa ikiwa hatutumiwe kile tulicho nacho kuwasilisha sayansi na
kuifanya iwe ‘fashionable’?”
Amehimiza waandishi wa habari kutumia vema
majukwaa ya kidigitali kama fursa ya kufikisha taarifa muhimu zinazohusu
sayansi kwa kundi la vijana ambalo kubwa lipo kwenye majukwaa hayo.
"Kila mtu yupo TikTok, kila mtu yupo
YouTube, lakini lazima tuone maudhui ya sayansi pia kwenye TikTok au YouTube.
"Tumia majukwaa haya maarufu kuwasilisha
sayansi. Tuwafikie vijana walipo kwenye YouTube, Instagram na mitandao mingine
na kuwapa elimu ya sayansi kwa njia wanayoielewa.”
Picha zote kwa hisani ya DSTI



0 Maoni