Kauli ya Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki
Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima,imezua taharuki nchini, ikitafsiriwa na
wachambuzi wengi kama kauli za uchochezi zaidi kuliko kuponya.
Kauli hiyo wanasema wachambuzi inaonekana kuhalalisha matukio ya ghasia ya
Oktoba 29 kwa kuyaita "maandamano" badala ya uhalifu.
Wachambuzi hao wakielezea kuhusu
mkutano wake na waandishi wa habari ulioenda mubashara, kwamba mazungumzo yake
yalionekana kwenda kinyume na wito wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa
maridhiano na amani.
Wachambuzi wameeleza kusikitishwa
kwao na namna ambavyo kiongozi huyo, kwa kutumia mgongo wa Kanisa, anajaribu
"kum pre-empt Rais" na "kuua ujumbe wa amani" kwa kutoa
kauli zake mubashara muda mfupi tu kabla ya Mkuu wa Nchi kufanya mikutano
muhimu. Hoja hii inaashiria mlengo na ajenda ya kisiasa.
Kwa mujibu wa maoni ya mtandaoni,
baadhi ya wachambuzi wamekumbusha maneno ya Maandiko Matakatifu wakisema:
"IMEANDIKWA HERI YAO WAPATANISHI " na hivyo wanamshangaa kiongozi
huyo wa kanisa badala ya kujikita kupatanisha anatoa maneno ya kuwasha moto na
hivyo kuibua maswali mazito kuhusu wajibu wa Kanisa: je, tunataka kuona taifa
letu likitumbukia kwenye shimo la machafuko?
Aidha wachambuzi hao wanasema mdudu
hatari anayeitwa udini pia anaonekana kunyemelea kutokana na kauli za kiongozi
huyo wa kanisa. Kuhoji kwanini viongozi wenzao wa dini nyingine hawakulalamika
mauaji yaliyotokea miaka ya nyuma, kunathibitisha kuwepo kwa uadui unaohama
baina ya viongozi wa dini na wafuasi wao, jambo linalotishia umoja na mshikamano
wa kitaifa.
Wakati taifa linahitaji uponyaji na
kukumbatia amani, wachambuzi wanamtaka Padri Kitima na wenzake kutambua wajibu
wao wa kihistoria. "Viongozi wa dini msigeuze kuaminika na kuaminiwa kuwa
fursa ya kutugawa na kuchochea chuki,"
baadhi ya waumini wenyewe wa kanisa hilo wameandika.

0 Maoni