Jeshi la Polisi Mbeya linamshikilia Mussa Basuka (30) mchimbaji mdogo wa madini, mkazi wa Manyanya Wilayani Chunya kwa tuhuma za mauaji ya rafiki yake aitwaye Issa Mohamed (30) ambaye naye ni mchimbaji mdogo wa madini na mkazi wa Kitongoji cha Manyanya Wilayani Chunya mkoani Mbeya.
Chanzo cha tukio hili ni mzozo uliotokea baina yao wakiwa kwenye chumba walichopanga uliotokana na ulevi wakibishania zamu ya kupika chakula cha jioni ambapo marehemu alikuwa na jukumu la kupika na mtuhumiwa alikuwa na jukumu la kuchotamaji.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mbeya ACP Wilbert Siwa amesema tukio hilo limetokea Februari 18, 2025 katika Kitongoji cha Manyanya, Wilaya ya Chunya baada ya mtuhumiwa Mussa Basuka (30) kumpiga ngumi kichwani rafiki yake aitwaye Issa Mohamed (30) ambaye walikuwa wakiishinaye chumba kimoja.
0 Maoni