Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kupitia
Wizara ya Maliasili na Utalii wamepiga kambi Mkoani Tanga, Wilaya ya Korogwe
kijiji cha Kwaisewa na Wilayani Mkinga kijiji cha Kwangena vinavyokabiliwa na
changamoto ya Mamba.
Timu hii ya wataalamu wanaendelea kutathmini athari na
madhara yaliyojitokeza kutokana na uwepo wa Mamba katika maeneo ya moto wananchi
wanapopata huduma ya maji. Tathmini
imefanyika kwa kushirikiana na wananchi na ujenzi wa vizimba unaendelea katika
maeneo husika.
TAWIRI imefanya tathmini ya maeneo husika kupitia vikao na
viingozi wa Wilaya na vijiji husika ili kuondoa adha hii, kizimba Kimoja
kitajengwa kijiji cha Kwaisewa - Korogwe Katika Mto Pangani - Ruvu eneo la
Lang'ata na Kizimba kimoja kijiji cha Kwangena Wikayani Mkinga, pembezoni mwa
mto Zigi.
Maeneo haya ni maeneo muhimu sana ambapo wanajamii hupata
huduma ya maji kila siku kwa matumizi ya binadamu na mifugo lakini pia ni
maeneo hatarishi kwa mamba. Wananchi hawa kwa sasa hawana huduma ya maji ya Bomba wala visima hivyo
hutegemea makji ya mto.
Akishukuru kwa niaba ya viongozi, Mhe. Aloyce Kundema,
Diwani wa Kata ya Mnyenzini Wilaya ya Mkinga, alisema hakika msaada huu umekuja
muda muafaka kwani wananchi wengi hasa watoto wamepoteza maisha na wengine
kupata vilema vya kudumu kufuatia adha ya Mamba. Aidha amepongeza juhudi za
Wizara ya Maliasili nanutalii kuleta.msaada huu, anaamini hii itakuwa suluhu
hasa katika kuokoa maisha ya wananchi.
Kazi hii inategemewa kukakimilika ndani ya wiki mbili, vizimba vitakabidhiwa rasmi kwa viongozi husika ngazi ya Wilaya, na elimu zaidi ya matumizi ya vizimba, na namna ya kujiokoa dhidi ya uvamizi wa Mamba itaendelea kutolewa.
0 Maoni