Mvua kubwa inayoambatana
na kimbunga Helene imeleta madhara katika maeneo ya North Carolina na Tennessee kusini mashariki
mwa Marekani na kusababisha vifo vya watu 59.
Mji wa
mlimani wa Asheville uliopo North Carolina umetenganishwa na mafuriko katika
siku ya Jumamosi.
Watu zaidi
ya 400 wamelazimika kutotoka nje katika jimbo hilo, ambalo watu 10 wamekufa.
Mahitaji ya kila siku yamelazimika kupelekwa kwa njia ya anga, amesema Gavana
wa jimbo hilo Roy Cooper.
Maafisa
wameendelea kufanya uokoaji kwa kutumia boti, helkopta na magari makuwa kusaidia
watu waliokwama kwenye mafuriko.
Wafanyakazi
wapatao 50 na wagonjwa wao wamelazimika kujikusanya juu ya paa la jengo la hospitali
ya Tennesse.
0 Maoni