Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi, Dkt. Asha-Rose Migiro amefungua Jukwaa la Wanawake 2025, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC), lenye kauli mbiu 'Mama ni Amani’, leo Alhamisi, tarehe 4 Desemba 2025, jijini Dodoma.
Jukwaa hilo lililowakutanisha wanawake walioko kwenye
makundi ya kijamii kutoka maeneo mbalimbali nchi nzima, pia lilihudhuriwa na
viongozi wa dini pamoja na wageni wengine waalikwa, lengo likiwa ni kuzungumzia
mchango wa wanawake katika kudumisha tunu zinazojenga misingi ya taifa na
kuimarisha nchi yetu.




0 Maoni