Klabu ya Soka ya Yanga Sc imetinga fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuichabanga Marumo Gallants goli 2 kwa 1.
Yanga wametinga fainali kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa timu hiyo baada ya ushindi wa jumla wa goli 4-1 dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika ya Kusini.
Marumo Gallants ambao ni wenyeji katika mechi ya leo wameshindwa kuonesha umwamba mbele ya wageni Yanga ambao nyumbani waliwachapa goli 2-0
Magoli ya Yanga yamefungwa na Fiston Mayele dk 45 ya kipindi cha kwanza na la pili likifungwa na Kennedy Musonda dk 62.
Yanga sasa wanasubiri mshindi kati ya Asec Memosa vs USM Alger.
5 Maoni