Waliohusika vifo watoto mapacha wasimamiswa kazi


 

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema serikali imechukua hatua ikiwemo kusimamishwa kazi kwa wahudumu wanaodaiwa kufanya uzembe hadi kifo cha mapacha waliozaliwa.


Waziri Ummy amejibu hoja  hiyo baada ya kuenea taarifa mtandaoni kuhusu tukio hilo amesema “Tumelifuatilia  suala hili, kuna ukweli. Uongozi wa (W) Kaliua umeshaanza kuchukua hatua, baadhi ya Watumishi wa Afya waliomuhudumia mama huyu wameshasimamishwa kazi.

Hata hivyo amekemea vikali kitendo hicho na kumuagiza mganga mkuu mkoani Tabora  kusimamia vyema Weledi,Maadili na Miiko ya Watumishi wa afya.


Taarifa hiyo ilienea zaidi mtandaoni ikieleza namna ambavyo mapacha hao waliozaliwa njiti walifariki kwa uzembe wa wahudumu huku kukiwa na utata namna ambavyo watoto hao walihudumiwa.

Undani wa tukio hilo uko hapa 👇🏾👇🏾👇🏾








Chapisha Maoni

0 Maoni