Waziri Mkuu Majaliwa amaliza utata mgomo wa Kariakoo, tume ya watu 14 yaundwa


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaomba wafanyabiashara kurejea kufanya biashara katika Soko la Kimataifa la Kariakoo baada ya kugoma kwa muda wa siku tatu mfululizo.

Waziri Mkuu Majaliwa  ametoa ombi hilo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Kimataifa la Kariakoo katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam amesema kuwa uamuzi wa kurejea kufanya biashara ni wenye kuleta tija kwa taifa na kwa uchumi.


“Tunajua Wafanyabiashara wana Mikopo, wanahitaji kupanua Biashara, Siku nne zilizopotea ni nyingi mno, nawaomba sana sana tuwarudishe Wafanyabishara walioondoka na kuhama Soko la Kariakoo” amewasihi wafanyabiashara



Waziri Mkuu Majaliwa amesema hoja zote zilizozungumzwa na Wafanyabishara zinaendelea kufanyiwa  kazi na kuwa itaundwa tume ya watu 14


“Lakini mfumo upi utafanyia kazi, ni shirikishi, kazi hiyo si ya Serikali pekee, lazima tuwe na Tume ya pamoja Tume ya kuangalia jinsi ya kusaidia kutatua ufumbuzi wa nini kifanyike kuhusu changamoto za kibiashara itakuwa na watu 14” amesema Waziri Mkuu



“Na tume hii itakuwa na watu 14, ambapo 7 kutoka serikalini na 7 kutoka kwenu, nataka nyie muunde timu ambayo itakwenda kukaa na viongozi wa serikali, timu hii ndani ya wiki mbili inatakiwa ipitie na ichukue yote waainishe, yatachakatwa na mrejesho mtapewa" Waziri Mkuu


Alisisituza agizo la kuvunja Kikosi Kazi lipo palepale, TRA walileta vijana ambao hawajasomea kazi ya kodi,wamekuja vijana ambao wana tamaa zao za maisha. Hapana, haikubaliki!


Kuhusu polisi kukamata wafanyabiashara na kudai wameagizwa na TRA Waziri Mkuu Majaliwa amesem “Kodi zitakusanywa na Maafisa wa TRA ambao wamesomea na wana maadili ili wakikosea tuwabane”


Awali Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka wafanyabiashara hao kusema kwa uwazi changamoto zinazowakabili hata kama ikimaanisha kumkosoa yeye, akisisitiza kwamba hakuna atakayedhurika kwa atakachosema. 



Kwa upande wao Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoa wa Tanga Ismail Masoud, amesema kama wananchi wanaumizwa na ubadhirifu wa fedha za umma unaofanyika Srikali na kuwa watafanya dua ya Albadiri kwa ajili ya wanaoiba.


“Hakuna mfanyabiashara anayetamani kufanya biashara kwa fujo, na ndo maana wafanyabiashara ni wepesi kutoa rushwa ili akae kwa amani, lakini kama mazingira ya amani yakiwekwa hakuna mtu ambaye atatoa rushwa.”

Chapisha Maoni

0 Maoni