Fred Vunjabei ashindwa kuvumilia mgomo Kariakoo

 


Wafanyabiashara wakubwa na wadogo katika soko la Kimataifa la Kariakoo wametoa yamoyoni mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.


Miongoni mwa wafanyabiashara waliopata nafasi ya kutoa maoni yao ni Fred Ngajilo maarufu “Vunjabei” amesema dhima ya wafanyabiashara ni kulipa kodi lakini wasaidizi waserikali wanapokwenda kinyume taratibu na sheria ya kikodi ndio chanzo cha migomo iliyopo.



"Mimi ni mfanyabiashara wa duka la nguo lakini pia duka la dawa za binadamu tumefunga  maduka mpaka sasa tunashindwa kufanya biashara lakini sio kwa sababu tunapenda. Kuna watu hapa wa kipato cha chini ambao anafanya kazi kuanzia asubuhi jioni ndio apate hela ya kula asipouza analala njaa"


Amesema Kwenye matatizo hayo  ipo mizizi miwili ambayo ndiyo chanzo cha haya yote ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa Elimu kwa mlipa kodi. “Tangu naingia Kariakoo hakuna hata siku moja niliwahi kuona mafunzo ya kodi kwa wafanyabiashara. Tunaomba Wafanyakazi wa TRA waje na wao kufungua maduka tuwasimamie tuone kama watatoboa hata miezi mitatu"  amesema 


Kauli hiyo ilizua shangwe na kusema “hawa wanaopiga makofi ni watu wa chini sana TRA kuna muda unakuta duka lina mtaji wa Milioni 3 mtu anapewa faini ya Milioni 3.5.

“Niliwahi kushuhudia mama mmoja amekabidhi kila kitu cha dukani mpaka TIN number akasema hatokaa afanye biashara tena kwa sababu TRA hawaangalii uwezo wa mfanyabiashara kulipa" - Amesema Mfanyabiashara Ngajilo

Chapisha Maoni

0 Maoni