Mabaki ya moja ya meli maarufu duniani ya Titanic
yamebainika vyema kwa mara ya kwanza tangu meli hiyo izame miaka 111 iliyopita.
Picha kamili ya digitali ya Titanic, ambayo imezama chini baharini
mita 3,800 katika eneo la Atlantic, imepiigwa kupitia vipimo vya kina kirefu.
Picha hiyo ya teknolojia ya 3D inaonyesha meli hiyo yote,
kwa muonekano wa kama vile maji yameondolewa.
Ni matumaini sasa itawezekana kupata jawabu la nini haswa
kilitokea kwenye meli hiyo kubwa wakati ilipozama mnamo mwaka 1912.
Watu zaidi ya 1,500 walikufa wakati meli hiyo ilipogonga
pande la barafu ikiwa katika safari yake ya kutoka mji wa Southampton, England hadi New
York, Marekani.
0 Maoni