Rais Samia aipongeza Yanga kutinga fainali

 


Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza Klabu ya Yanga kwa kutinga faina CAFCC.

Kupitia ukurasa wake mtandao wa twita Rais Samia ameandika “Pongezi za dhati kwa Klabu ya Yanga kwa kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup). Mmeandika historia na kuipa nchi yetu heshima kubwa sana. Nawatakia kila la kheri katika mchezo wenu wa Fainali”



Klabu ya Soka ya Yanga Sc imetinga fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuichabanga Marumo Gallants goli 2 kwa 1.


Yanga wametinga fainali kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa timu hiyo baada ya ushindi wa jumla wa goli 4-1 dhidi ya Marumo  Gallants ya Afrika ya Kusini.


Ushindi wa kihistoria wa Yanga unawafanya waondoke na kitita cha milioni 20 kutoka kwa Rais Samia ikiwa ni motisha kwa kila goli litakalofungwa katika mashindano ya timu hiyo kimataifa.


Mapema akizungumza na wafanyabiashara Mnazi mmoja Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa aliahidi mapokezi mazito kwa timu hiyo kuanzia uwanja wa ndege endapo itatinga fainali.



Chapisha Maoni

1 Maoni

Bila jina alisema…
asante mama