Yanga yaweka historia yatinga fainal CAFCC

 

Klabu ya Soka ya Yanga Sc imetinga fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuichabanga Marumo Gallants goli 2 kwa 1.


Yanga wametinga fainali kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa timu hiyo baada ya ushindi wa jumla wa goli 4-1 dhidi ya Marumo  Gallants ya Afrika ya Kusini.



Marumo Gallants ambao ni wenyeji katika mechi ya leo wameshindwa kuonesha umwamba mbele ya wageni Yanga ambao nyumbani waliwachapa goli 2-0


Magoli ya Yanga yamefungwa na Fiston Mayele dk 45 ya kipindi cha kwanza na la pili likifungwa na Kennedy Musonda dk 62.


Yanga sasa wanasubiri mshindi kati ya Asec Memosa vs USM Alger.

Chapisha Maoni

5 Maoni

Bila jina alisema…
Sisi ndo yangaaaqqq
Bila jina alisema…
Yanga pigaaaqq haoooo
Bila jina alisema…
Yanga taifa kubwa yanga mashine
Bila jina alisema…
Yanga sasa wamekamata kila konaaaq
Bila jina alisema…
Yanga wabutua waweka historia