Marekani na Urusi waanza mazungumzo vita ya Ukraine

 

Marekani na Urusi wanafanya mazungumzo Saudi Arabia kuhusiana na vita vya Ukraine, ukiwa ni mkutano wao wa kwanza wa ana kwa ana, baina ya mataifa hayo tangu Moscow iivamie Ukraine.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov anakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio Jijini Riyadh, lakini si Ukraine ama taifa lolote la Ulaya lililoalikwa.

Marekani inasema kwamba mazungumzo hayo ni hatua ya kwamza kuona iwapo Urusi inadhamira ya dhati ya kumaliza vita, wakati Urusi ikisema lengo ni kuweka sawa uhusiano na Marekani.

Hata hivyo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hatotambua makubaliano yatakayofikiwa katika mazungumzo ambayo haijahusishwa. Viongozi wa Ulaya pia wanataka kushirikishwa, na jana walifanya mkutano wa dharura.



Chapisha Maoni

0 Maoni