Abiria wote 80 pamoja na wahudumu wa ndege iliyoanguka na kupinduka wakati ikitua kutokana na hali mbaya ya hewa kwenye uwanja wa ndege wa Toronto Pearson nchini Canada wamenusurika kifo.
Taarifa zinasema kwamba ndege hiyo aina ya CRJ900 iliyotengenezwa Canada miaka 16 iliyopita na kampuni ya Bombardier ilikuwa na na abiria 76 na wahudumu wanne wakati ikianguka.
Abiria 18 wamepelekwa hospitali. Mtoto, mwanaume mwenye
umri wa miaka 60 na mwanamke wa miaka 40 wameumia vibaya, imeeleza taarifa ya
kampuni ya magari ya wagonjwa ya Ornge ya Otario.

0 Maoni