Mwenyekiti
wa bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Jenerali Venance
Mabeyo (Mst) amewavisha cheo makamishna wasaidizi waandamizi wa uhifadhi wawili
na kuwahimiza Kuchapa kazi, uadilifu, kutimiza wajibu, kuzingatia sheria,
kanuni na taratibu zinazoongoza utendaji kazi katika utumishi wa Umma.
Waliovishwa
Cheo baada ya kuhitimu mafunzo ya Jeshi la Uhifadhi ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Uhifadhi Brown O. Shimwela anayesimamia Idara ya fedha pamoja na Kamishna
msaidizi Mwandamizi Dkt. Amani Makota anayesimamia Idara ya TEHAMA na Takwimu.
Baada ya
kuwavisha vyeo Jenerali Mabeyo ambaye
pia ni Mkuu wa Majeshi Mstaafu amewasisitiza viongozi hao wapya kushirikiana na
Menejimenti ya Ngorongoro kuboresha zaidi miundomninu ya utalii, kuboresha
huduma kwa wateja, kubuni mazao mapya ya utalii, na kusimamia kikamilifu maeneo
ya malikale yaliyopo nje ya eneo la Ngorongoro kama Mapango ya Amboni na
Kimondo cha Mbozi ili rasilimali hizo za malikale ziongeze mchango katika pato
la taifa.
“Tuboreshe
huduma za wageni ikiwemo miundombinu ya utalii, vivutio vya malikale kama
mapango ya ambone na Kimondo cha Mbozi,
tubuni mazao mapya ya utalii, kuyaendeleza na kuyatangaza ili kuwe na mtawanyiko wa wageni wanaotembelea hifadhi,
uboreshaji wa miundombinu uende sambamba na kuimarisha mifumo ya TEHAMA
iendelee kusomana kwa ajili kuongeza kwa Taifa letu na watanzania kwa Ujumla,”
amesisitiza Mabeyo.
Kamishna
wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bw. Abdul-Razaq Badru ameleza
kuwa makamishna hao wapya kuungana na Menejimenti ya Ngorongoro ni sehemu ya
kuongeza nguvu kazi katika utekelezaji wa majukumu ya kusimamia Uhifadhi,
utalii na Maendeleo ya Jamii kikamilifu katika kukuza uchumi wa Nchi.
Badru
ameongeza kuwa Utalii ni sekta kinara katika kuchangia uchumi ya Nchi, hivyo
mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa kushirikiana na Wadau wa utalii inaendelea
kuongeza mazao mapya ya utalii na kuyatangaza ili kuongeza idadi ya watalii
na pato la taifa.
Na.
Kassim Nyaki- NCAA




0 Maoni