Tanzania imejengwa juu ya misingi ya Sheria, utawala
bora, na siasa za hoja. Hata hivyo, mwenendo unaoendelea ndani ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) unadhihirisha dalili za chama kilichopoteza
dira, kikigeuza uvunjaji wa Sheria kuwa "mkakati" wa kujitafutia
huruma ya kisiasa.
Kile kilichokuwa chama chenye 'Think-Tank' imara na
hoja za kitaalamu, sasa kinaonekana kuishiwa ubunifu. Badala ya kuja na
mikakati ya kiufundi na kisera, tunashuhudia mbinu za kutengeneza
"kiki" mitandaoni:
Kuvunja Sheria Makusudi:
Wafuasi wanavuka mipaka bila vibali, wanafanya
vitendo vya kihuni, au kuanzisha vurugu nje ya Mahakama, kisha wakikamatwa,
wanageuza tukio kuwa propaganda za "tumeonewa."
Kisa cha Kuhuzunisha:
Kisa cha hivi karibuni cha mwanachama wa Chadema
kumvamia askari nje ya Mahakama Kuu ni mfano wa wazi wa siasa iliyofilisika;
inajaribu kutengeneza "huruma" badala ya kutoa hoja.
UKWELI NI HUU:
Uongozi wa kisiasa si kinga dhidi ya Sheria. Sheria
haipendelei chama, haina rangi ya bendera, ni msumeno unaokata kote. Mwanasiasa
anayevunja Sheria ana wajibu wa kuwajibika kama raia mwingine yeyote.
Kujenga hadithi ya "tunadhulumiwa" kila
mara siyo siasa, bali ni kuhalalisha utovu wa nidhamu na uvunjaji wa Sheria
makusudi. Siasa za hoja zinahitaji maarifa, si matusi. Zinahitaji mikakati, si
misemo ya huruma.
Kuvunja Sheria makusudi ili ukamatwe ni ujanja wa
muda mfupi unaodhihirisha kuishiwa kimkakati, si siasa ya maendeleo, bali ni
vioja vya kukosa dira.
Tanzania inahitaji upinzani makini unaotoa hoja
zenye mashiko.Turejee kwenye misingi ya uwajibikaji na nidhamu ya kisiasa.

0 Maoni