Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) ameisisitiza UVCCM kuendeleza kasi ya uhamasishaji uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura na kuhakikisha vijana wengi wanajiandikisha litakapoanza kwa upande wa Unguja hivi karibuni.
Ametoa wito
kwa vijana kutobaki nyuma siku ya kupiga kura ili CCM ipate ushindi wa
kihistoria na kuendelea kushika Dola.
Dkt. Mwinyi
ameyasema hayo alipozungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la Bweni la Vijana
wa Kiume wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).
Aidha Dkt. Mwinyi
ameeleza kuwa ni lazima Chama nacho kiache alama ya uongozi itakayokumbukwa kwa
muda mrefu kwa kufanya mambo makubwa ya maendeleo na miradi ya Chama katika
ngazi zote.
Halikadhalika
Dkt. Mwinyi amefahamisha kuwa alama iliyoachwa na Serikali katika Sekta zote za
Maendeleo ni lazima pia iachwe ndani ya CCM.
Vilevile Dkt.
Mwinyi ameipongeza UVCCM kwa kufanikiwa kujenga Jengo hilo litakalotumika kwa
harakati mbalimbali za Jumuiya hiyo.
Kwa upande
mwingine Dkt. Mwinyi amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuunga Mkono
juhudi za Jumuiya hiyo kwa hali na Mali ili dhamira ya kuwajenga vijana kuwa
wazalendo na kuwapatia mafunzo mbalimbali ifanikiwe.
Naye
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Taifa, Mohammed Ali Kawaida amesema Kauli ya
Mitano Tenani kwa ajili ya viongozi wawili tu ndani ya CCM ambao ni Mwenyekiti
wa CCM Taifa, Ndugu Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Mwenyekiti CCM Zanzibar,
Ndugu Hussein Ali Mwinyi.




0 Maoni