Yanga yaichakaza Marumo Gallants 2-0

 

Klabu ya Yanga imewachakaza Marumo Gallants ya Afrika ya kusini goli mbili kwa nunge.



Ni Katika mchezo wa raundi ya kwanza ya hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho Afrika, Magoli ya Yanga yamewekwa kimiani na Stephane Aziz K dk 64 na Benard Morrison dk ya mwisho ya mchezo.


Timu zote mbili zilicheza kimbinu katika dk 90 na Yanga wakiitumia mbinu na kuhakikisha wanaingia kimiani mara mbili. 



Kipindi cha kwanza Yanga wametoka na kadi mbili za njano, kipindi cha pili Yanga walibadilisha wachezaji wa tano na hivyo kituo kinachofuata ni kwa madiba Afrika ya Kusini mechi inayotarajiwa kupigwa Mei 17, 2023.

Chapisha Maoni

3 Maoni

Bila jina alisema…
Wape salamu zaooooo
Bila jina alisema…
Wacha waone wenyewe wameyakanyagaaaa
Bila jina alisema…
Watahadithiaaa leo