Golikipa nguli aliyecheza mara tano kombe la dunia afariki

 

Nguli  wa soka raia wa Mexico golikipa Antonio Carbajal, mwanasoka wa kwanza kucheza katika Kombe la Dunia matano, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 93.


Carbajal raia wa Mexico anayejulikana kama El Cinco Copas baada ya mafanikio yake, alicheza Brazil 1950, Uswisi 1954, Sweden 1958, Chile 1962 na England 1966 Kombe la Dunia.

Carbajal alishikilia rekodi hiyo peke yake kwa miaka 32 hadi ilipofikiwa na Lothar Matthaus wa Ujerumani mwaka 1998.

Aliichezea nchi yake mechi 48, 11 kati ya hizo zilicheza Kombe la Dunia, pamoja na mechi 409 katika ngazi ya vilabu.


Chapisha Maoni

0 Maoni