Waziri Nape aomba 212. 4 bilioni bajeti 2023/24

 

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameomba bunge kuidhinisha  jumla ya Shilingi 212,457,625,000 Katika Mwaka wa Fedha 2023/24.


Waziri Nape ametoa ombi hilo wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2023/24 na kueleza Kiasi cha Shilingi 30,503,685,000 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambapo Shilingi 18,522,155,000 ni za Mishahara na Shilingi 11,981,530,000 ni za Matumizi Mengineyo; na Kiasi cha Shilingi 181,953,940,000 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ambapo Shilingi 146,777,440,000 ni Fedha za Ndani na Shilingi 35,176,500,000 ni Fedha za Nje.


Akizungumzia  utekelezaji wa bajeti iliyopita Waziri Nape amesema Mwaka wa Fedha 2022/23 Wizara iliidhinishiwa kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 282.06, Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 26.3 ziliidhinishwa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi bilioni 255.8 ziliidhinishwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. 

Hata hivyo hadi kufikia mwezi Aprili, 2023 Wizara imepokea na kutumia jumla ya Shilingi bilioni 125.1. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 12.8 sawa na asilimia 48.7 ya fedha za matumizi ya kawaida na Shilingi bilioni 112.3 sawa na asilimia 43.9 ya fedha za mendeleo.


Awali akitoa mipango ya Wizara hiyo amesema Wizara hiyo imedhamiria kuharakisha nchi kuelekea katika uchumi wa kidijitali hususan kuhimiza mfumo wa kufanya biashara bila fedha taslimu (cashless economy), ambao unaowezeshwa na kuendeshwa na TEHAMA.


“Ili kufanikisha haya kwenye sekta zote za uchumi na kijamii, Wizara imepanga kufanya mabadiliko na maboresho makubwa kwenye sekta ili kuendana na mageuzi haya ikiwemo kuharakisha ujenzi, uendelezaji na usimamiaji miundombinu ya habari, mawasiliano na teknolojia ya habari”


Makusanyo 

Waziri Nape Nnauye amesema katika Mwaka wa Fedha 2023/24, Wizara inakadiria kukusanya Sh bilioni 150.7 fedha hizo zitatokana na mauzo ya huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, tozo itokanayo na kuongeza salio la simu na usajili wa Magazeti.


Maeneo mengine wanayotarajia kukusanya fedha hizo kutoka katika ada ya mwaka ya Magazeti, vitambulisho vya Waandishi wa Habari na machapisho ya picha pamoja na mabango na majarida.



Makusanyo hayo ni zaidi ya makadirio ya mwaka 2022/23 ambapo hadi kufikia kufikia tarehe 30 Aprili, 2023 Wizara imekusanya jumla ya Shilingi bilioni 24.9 kutokana na mauzo ya huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, tozo kuongeza salio, mauzo ya picha za Viongozi Wakuu wa nchi, machapisho na ada ya mwaka ya magazeti.


Maboresho 

“Ili kufanikisha haya kwenye Sekta zote za Uchumi na Kijamii, Wizara imepanga kufanya mabadiliko na maboresho makubwa kwenye Sekta ili kuendana na mageuzi haya ikiwemo kuharakisha ujenzi, uendelezaji na usimamiaji miundombinu ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,” amesema  waziri Nape


Aidha, amesema  wizara itafanya mapinduzi kwenye taasisi za sekta kwa kuimarisha mashirikiano na Sekta binafsi, kuendeleza tafiti na ubunifu kwenye masuala ya TEHAMA ikiwemo uanzishwaji na uendelezaji wa kampuni changa (startups), kuwezesha Sekta nyingine kuelekea kwenye mapinduzi ya kidijitali; na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari.

Chapisha Maoni

4 Maoni

Bila jina alisema…
Nape make media great again
Bila jina alisema…
Hapa sasa tozo vyombo vya habari ziondolewe kabisa
Bila jina alisema…
Maisha yameanza kwa vyombo vya habari
wavisaidie vile ambavyo vinakufa
Bila jina alisema…
Mzee wa bao la mkono anaonesha mkono wake