Jacob Wekesa, anayejiita mtume, ameingia matatani baada ya
kufikishwa Mahakamani Kenya kwa mashtaka ya kuwabaka mabinti wawili wa muumini
wake aliyemkaribisha nyumbani kwake ‘mtume’ huyo na kukaa naye.
Wekesa wa kanisa la Legion of Mary, alikaribishwa kwa
muumini wake Sarah Otieno huko Njoro, ambapo akiwa nyumbani kwa mwenyeji wake
aliwarubuni mabinti wawili wa muumini wake na kuwabaka.
Mtume huyo feki, amekuwa akidai kuwa anauwezo wa kubaini
mwanamke mwenye matatizo ya kupata ujauzito kwa kutumia macho yake yenye uwezo
wa kiroho, na kumtibu ili aweze kushika mimba na kuza.
Mmoja wa watoto hao wa kike alieleza kuwa Wekesa alimuita chumbani
kwake ambacho kilikuwa kinapakana na chao na kumuambia anamatatizo ya kukosa
ujauzito na kisha akaanza kumtomasa na kisha kumbaka na kumuonya asipige
mayowe.
Baada ya kumfanyia kitendo hicho, alimuambia avae nguo zake
kwani amesha pona na kumuonya kuwa asimwambie mtu yeyoye, kwani kunawatu wengi
amewafanyia hivyo na wamekaa kimya na wamepona tatizo lao.
Hata hivyo Binti huyo hakukaa kimya alimueleza dada yake cha
kushangaza dada naye aliangua kilio na kusema ‘mtume’ huyo pia amembaka na yeye
kwa njia hiyo hiyo, ndipo walipoenda hospitali na daktari kuthibitisha kuwa
wamefanyiwa ukatili wa kingono na kuwapatiwa dawa.
Katika utetezi wake Wekesa alidai kuwa asingeweza kuwabaka mabinti
hao kwa kuwa walikuwa wanaondoka nyumbani alfajiri na kurudi usiku wa manane,
na kuongeza kuwa amebambikiziwa kesi hiyo.
Hata hivyo Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Edward Obonge
amemtia hatiani Wekesa kwa kosa la ubakaji na imepanga kutoa hukumu ya kesi
hiyo Juni 6, mwaka huu.
0 Maoni