Rais Samia ahimiza uwekezaji kwenye rasilimali watu

 

Rais Samia Suluhu Hassan amesema viongozi wa Afrika wanapaswa kuwekeza kwenye rasilimali watu ili kuharakisha ukuaji wa uchumi, kuongeza tija kwa vijana na wanawake kwa kuboresha mafunzo na ujuzi. 


Rais Samia ameyasema hayo wakati kuzindua Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali watu (Africa Heads of State Human Capital Summit) utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 25 hadi 26 mwaka huu.



Akizindua mchakato huo, Rais Samia

amesema ni muhimu kwa viongozi wa Afrika kuwekeza kwenye rasilimali watu kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi barani humo iendani na kauli mbiu inayosisitiza  kuharakisha ukuaji wa uchumi wa Afrika, kuongeza tija kwa vijana kwa kuboresha mafunzo na ujuzi.


Rais Samia amesema Afrika bado haijawekeza vya kutosha kwenye rasilimali watu hususani chini ya Jangwa la Sahara, “ni muhimu kwetu viuongozi kuendelea kuwekeza kwa watu husani vijana na wanawake kwa kuhakikisha sera zinazotungwa zinaimarisha ubora na uwezo wa watu wao.”Amesema



Amesema, kwa mujibu ripoti ya Umoja wa Mataifa inaonesha kuwa nchi za Afrika zinakabiliwa na changamoto ya kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) hivyo ni fursa kwa wakuu wa nchi kujadili na kubadilisha uzoefu kuhusu mchango wa rasilimali watu katika ukuaji wa uchumi na maendeleo.


Kwa upande wake Mkurugenzi   Mkazi wa Benki ya Dunia, Nathan Belete, amesema takwimu zinaonesha asilimia 70 ya vijana wa kiafrika wanafanya kazi kwenye sekta isiyo rasmi na yenye kipato kidogo.



Kwa mujibu wa Balete nchi za Afrika zinapaswa kufanyia kazi zaidi changamoto ya rasilimali watu inayowakabili japo kuna jitihada kwa serikali zake kuhakikisha watoto wanakwenda shule, tatizo la ajira kwa vijana linapatiwa ufumbuzi.


Chapisha Maoni

0 Maoni