IGP Sirro sitasahau panya road,Kibiti

 

Mkuu wa zamani wa Jeshi la Polisi  (IGP) Balozi Simon Sirro amesema hatoweza kusahau matukio ya mauaji Kibiti  na wizi wa kutumia silaha katika kipindi cha uongozi wake.


Mstaafu IGP Sirro ameyasema hayo baada ya hafla kuagwa ambayo imefanyika Chuo Cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam mbali na kuwashukuru Watanzania kwa ushirikiano mkubwa waliompatia kipindi cha uongozi wake na kwamba katika kipindi chake matukio hayo na uhalifu wa kutumia siraha yakiwemo ya Panyaroad ni matukio ambayo hatayasahau.


IGP Sirro ameagwa rasmi baada ya kustaafu utumishi ndani ya jeshi kwa mujibu wa sheria mwezi Machi mwaka huu, hafla iliyoongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Jumanne Sagini, mbapo Sirro alipigiwa gwaride maalum la kuagwa, huku akisukumwa kwa gari maalumu la Polisi.


IGP Mstaafu Simon Sirro amelitumikia Jeshi la Polisi kwa kipindi cha miaka 30 tangu mwaka 1993 alipojiunga rasmi hadi kustaafu Machi mwaka huu na amekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi  na kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.


Julai 2022 Rais Samia Suluhu Hassan alimteua IGP  Simon Sirro kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Zimbabwe nafasi ya Sirro ikachukuliwa  na Camillus Wambura ambaye alipandishwa  cheo na kumteua kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP).

Chapisha Maoni

2 Maoni

Bila jina alisema…
Nasi hatutawez kukusahau kwa kuwakomesha
Bila jina alisema…
Haya sasa mkuu kapambanie Zimbabwe