Fistula inatibika sio kwa wanawake pekee wanaume watajwa


Mkurugenzi wa miradi ya kukabiliana na kudhibiti magonjwa AMREF Dk Ritha Mutayoba amesema  kuwa fistula inatibika na kuwataka wananchi kutojificha na kujitokeza ili kuweza kutibiwa.

Dk Ritha Mutayoba ametoa wito huo wakati wa mahojiano na TBC1 ikiwa ni siku ya Kimataifa ya kutokomeza Fistula Duniani ambapo amesema jamii imekuwa ikiwaficha waathirika wa ugonjwa huo na wengine kuhusisha imani za kishirikina jambo ambalo limezorotesha utoaji wa huduma stahiki kwa waathirika.

Amesema fistula ya uzazi inayozungumziwa ni tundu lisilolakawaida kwa sababu kiasili mwanamke hajaumbwa na tundu hilo ambalo kuleta madhara makubwa kwa mwanamke katika jamii.


Tundu hilo hutokea kwa mama wakati wa kujifungua ambapo hutokea kati ya kibofu cha mkojo lakini kinaungana na njia ya uke ndio maana likaitwa tundu lisilolakawaida.



Lakini tundu hilo linaweza kutokea kati ya njia ya uke na nijia ya haja kubwa hivyo humpelekea mama kutokwa na haja kubwa bila kujitambua.


Dk Mutayoba amesema dalili kubwa ambayo mwanamke anakutana nayo ni pamoja na kujikuta amelowana na uchafu wa mkojo au kinyesi bila kujitambua.


Ameeleza kundi kubwa la wajawazito wanaoathiriwa na ugonjwa huo ni wale ambao wamechelewa kwenda kujifungua kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo umbali wa vituo vya afya, na uzembe unaoweza kujitokeza wakati wa kumsaidia mama mzazi kujifungua.



Huu ni unaohusisha  kutokea kwa tundu au muunganiko usio sawa  kati ya viungo mbali mwilini ikiwe kuwepo kwa tundu  kati ya Njia ya Mkojo na Kibofu cha Mkojo, Tundu kati ya Njia ya Mkojo na Njia ya Haya Kubwa,Tundu kati ya Njia ya Mkojo na Utumbo Mkubwa.


Kutokana na mapungufu hayo matokeo yake husababisha  Kujizuia kukojoa, au Uchafu wa Haja Kubwa kutokea Njia ya Haja Ndogo 


Tafiti za afya zinasema kuwa fistula ni kwamba haiwapati wanawake pekee kama inavyodhaniwa lakini huweza pia kuwapata wanaume kwani zipo aina mbali mbali za Fistula ikiwa ni pamoja na RectoVaginal Fistula(RVF) kwa kimombo ambayo hii ni aina ya Fistula inayohusisha  Tundu kati ya Njia ya Haja Kubwa na njia ya mkojo  wa mwanamke.

 


Aina ya pili ni ColoVaginal Fistula(CVF)ni ile ambayo huhusisha Tundu kati ya utumbo mkubwa na njia ya mkojo ya mwanamke.

 

Aina ya tatu VesicoVaginal Fistula (VVF) Hii ni aina ya Fistula ambayo huhusisha Tundu kati ya kibofu cha Mkojo na Njia ya Mkojo ya mwanamke.


Kwa mujibu wa Dk Mutayoba miongoni mwa sababu za maambukizi hayo ni pamoja na Majeraha au tundu  ambalo hutokea wakati Mwanamke anajifungua,ambapo linaweza kusabibishwa na mgandamizo wa mtoto wakati  anatoka au wakati mama anasaidiwa kutolewa mtoto wakati anajifungua kwa Njia ya kawaida na mara chache  hii huhusisha matumizi ya vifaa vyenye ncha kali.


Akizungumzia kuhusu matibabu amesema kuwa unatibiwa kwa kufanyiwa upasuaji kisha kuzibwa sehemu ya tundu la Fistula na baada ya upasuaji  mwanamke atapewa dawa  mbali mbali ikiwemo za kuzuia na kutibu maambukizi mengine.


Maadhimisho ya Fistula kwa Tanzania yanafanyika mkoani Kigoma. 

Chapisha Maoni

6 Maoni

Bila jina alisema…
Wanaume wasaidieni wanawake
Bila jina alisema…
Jaman elimu zaidi itolewe
Bila jina alisema…
Mungu awasaidie
Bila jina alisema…
Elimu elimu jamani
Bila jina alisema…
Elimu ni muhimu jaman wanawake wanateseka sana
Bila jina alisema…
Huku kwetu watu hawajui heri wanaume nao wadakwe ili wajue umuhimu wankulea wanawake