Jaji Mkuu Mahakama imetua mzigo

 

Jaji Mkuu wa Tazania Prof. Ibrahim Juma amesema uteuzi wa majaji wa mahakama ya rufani utapunguza mzigo wa mlundikano wa mashauri mahakamani.


Prof. Juma amesema hayo wakati wa uapisho wa viongozi mbalimbali walioteuliwa na Rais Samia wakiwemo majaji sita wa mahakama ya rufani  majaji wa rufani 31 ambao ni idadi itakayosaidia katika kurahisisha kupunguza mashauri mbalimbali mahakamani.

“Historia ya kwanza ni pale Rais Samia ulipoapisha majaji wakafika 25 kwa sababu tulikuwa hatujawahi kuzidi majaji wa rufani 16 au 15, ukafanya historia ikafika 25, na leo wamefika 31”amesema Jaji mkuu 


Amesema ongezeko la majaji 6 itasaidia kupunguza mashauri na kwamba mpaka sasa kuna mashauri 5,626 ambapo kila jaji anashughulikia mashauri hayo na kwa sasa itapunguza idadi kutoka 800 hadi 600.


“Kwa  sasa kuna ongezeko la mashauri ya mirathi ambayo hayajafanyiwa maamuzi na kumekuwa na ongezeko la fedha katika akaunti maalumu ya mirathi.” amesema Jaji Mkuu


Amesema ni faida kubwa inayotokana na ongezeko hilo na mashauri yatatolewa maamuzi kwa wakati na wananchi wanapata huduma kwa haraka.


Kwa upande wake Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson amesema majaji hao wa rufani wanategemewa sana katika utoaji wa haki na kutocheleweshwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni