Rais Samia aanika mambo ya hovyo ya Mahakamani

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka watendaji wa mahakama kuwa na macho  makali kabisa ngazi za chini ili kutoa haki kwa wananchi katika mashauri yao kwa wakati.

Rais Samia ameyasema hayo Ikulu Chamwino Dodoma baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateuwa hivi karibuni  ambapo amesema “bado mambo huko yanaendelea hovyohovyo kwahiyo naomba mtupie macho huko chini ili wananchi wa kawaida wapate haki zao ".



“Tumesikia kesi ya Lindi kwamba wafugaji wamefanya makosa ya waziwazi wamekamatwa kwenye makosa jaji akasema nami nakwenda huko huko kutazama na kurudi akasema hawana makosa sasa utajiuliza kuna nini hapo,” amesema Rais Samia.


Rais Samia pia amesema ukisikiliza kesi za wanaokamatwa kwenye hifadhi za wanyama pori zikifika mahakamani mambo huwa ni magumu na kuwataka kutupia macho katika eneo hilo.

“Wafugaji ile pesa inafanya kazi kwelikweli kwa hiyo naomba mtupie macho huko chini wananchi wa kawaida wapate haki zao." amesema Rais Samia 

Chapisha Maoni

0 Maoni