Watano wafariki ajalini Tabora

 

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Costantine Bugambi amethibitisha vifo vya watu watano na wengine 13 kujeruliwa baada ya basi kugonga lori mkoani Tabora.


Taarifa ya kamanda Bugambi imeleza ajali ya kwanza ilitokea Mei 21, mwaka huu katika kijiji na kata ya Ilolangulu wilayani Uyui ikihusisha basi la kampuni ya Delux aina ya Tata lenye namba za usajili T 164 DEL likiendeshwa na dereva mwenye umri wa miaka 35 likitoka Kijiji cha Sawewe kwenye Barabara ya Tabora-Urambo.


Alisema basi hilo liligonga lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 584 DTL na kusababisha kifo cha dereva wa gari hilo mwenye umri wa miaka 54 mkazi wa Tabora. Dereva wa basi amekamatwa.


Bugambi amesema  katika ajali hiyo watu wanne walikufa papohapo na mmoja alifariki  wakati anakimbizwa hospitali na majeruhi 13 wanatobiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora.


Ajali nyingine ni ya gari aina ya Toyota Land Cruiser mali ya Mamlaka ya Maji Mkoa wa Geita lenye namba za sajili wa STL 9690 liligonga pikipiki yenye namba za usajili MC 483 BVL ambaye alikufa papohapo.


Chapisha Maoni

0 Maoni