Rais Samia akoleza moto fainal Yanga na USM kwa Mkapa

 

Mechi ya fainali ya kombe la Shirikisho Afrika, kati ya Yanga na USM Algers unatarajiwa kupigwa  Mei 28, 2023 katika Dimba la Mkapa,Dar es Salaam.


Kufuatia mechi hiyo inayosubiriwa na madhabiki lukuki Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameongeza hamasa amenunua tiketi 5000 lengo likiwa ni kuongeza hamasa na kutengeneza mazingira mazuri kwa Yanga kutwaa ubingwa wa huo na kuandika historia mpya kwenye soka la Tanzania.


Taarifa ya Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa imeeleza  Rais Samia amewataka wadau wengine kujitokeza kununua tiketi kwa ajili ya mchezo huo ili kuwapa nafasi mashabiki wengi zaidi kuhudhuria mchezo huo na Yanga kuutumia vyema uwanja wa nyumbani kwa nguvu ya mashabiki.



Kwa upande wa Yanga kupitia Afisa Habari  wake Ally Kamwe amesema “Najivunia sana uwepo wa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, mama ametupa Ndege, ameweka zawadi ya milioni 20 kwenye kila goli lakini kama haitoshi ametoa tiketi Elfu Tano (5,000) kwa mashabiki watakaokuja Benjamin Mkapa Stadium tarehe 28 hii”

kwakweli sisi Yanga tunamshukuru sana Mama na tunaahidi kuwa hatutamuangusha”

Chapisha Maoni

0 Maoni