Baadhi ya wateja wanaopata huduma mbalimbali ikiwemo
za utalii wamejumuika na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika
kuhitimisha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Wakiongozwa na maafisa mbalimbali wa Mamlaka hiyo
wadau mbalimbali waliotembelea ofisi za Maelezo (Information Centre) katika
Jengo la Ngorongoro Arusha wameipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa
kupokea ushauri kuhusu uboreshaji wa miundombinu ya utalii na kuufanyia kazi.
Afisa Utalii Mkuu na Masoko wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro bwana
Michael Makombe amesema katika kipindi cha siku saba mamlaka imeweza kukutana
na wateja na kupokea ushauri kuhusu miundo mbinu,mifumo ya Tehama, Ulinzi na
Usalama pamoja na mambo mengine.
Wiki ya huduma kwa wateja huadhimishwa ili kuwaleta
pamoja wadau na watoa huduma kwa lengo la kupokea mrejesho wa huduma
wanazozitoa ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Dhamira inayowezekana
(Mission Possible).



0 Maoni