Kupiga kura
si kitendo cha kuweka alama tu; ni msingi wa maamuzi na njia kuu ya kushiriki
katika kuamua mustakabali wa nchi.
Ukiangalia historia ya Uchaguzi nchini hasa ule wa Kura
Tatu wa mwaka 1958 kwa iliyokuwa Tanganyika, ambapo TANU ilikabiliwa na uamuzi
mgumu wa kushiriki au kususia uchaguzi wenye masharti ya kibaguzi, tunapata
mafunzo makuu matatu yanayoonyesha umuhimu
wa kupiga kura.
Kura ni zana
ya kufanya maamuzi ya kimkakati kwa taifa. Katika Mkutano Mkuu wa Tabora, baada
ya mjadala mkali, wajumbe wa TANU waliamua mwelekeo wa chama kwa kupiga kura
(kura 37 za kuunga mkono kushiriki dhidi ya 23 za kususia). Kitendo hiki
kinaonyesha wazi kwamba kura, hata iwe kwa idadi ndogo, ndiyo inakuwa njia ya
mwisho ya kuamua hatua ya kisiasa na kwa maamuzi hayo, walifanikiwa, kuleta
uhuru wa Tanganyika.
Kura yako,
kama kijana, inakuwezesha kuchagua mwelekeo wa serikali na kuamua ni vipi sera
zinazoathiri ajira, elimu, na huduma za jamii zitatekelezwa. Kususia kura ni
sawa na kutoa mamlaka yako ya kuamua na kukikabidhi chama hasimu ushindi bila
wewe kutumia haki yako.
Kura yako
inakuwezesha kuchagua mwelekeo wa serikali na nchi. Kama vile kura chache za
wajumbe wa TANU ziliamua kushiriki na kuleta uhuru, kura yako inaweza kuamua ni
nani na kwa vipi sera zinazoathiri ajira, elimu, na huduma za jamii
zitatekelezwa. Kususia kura ni sawa na kukikabidhi chama hasimu ushindi bila
jasho, kama alivyosema Mwalimu Nyerere.
Hoja kuu
iliyotumiwa na Mwalimu Nyerere na Sheikh Abdallah Rashid Sembe ilikuwa kwamba
kususia uchaguzi ingekuwa ni kujiingiza katika mtego wa adui . Walisisitiza
kwamba TANU ingedhoofika na ikakosa sauti katika maamuzi ya baadaye ikiwa
ingesimama pembeni.
Waliona
umuhimu wa kushiriki na kushinda viti ili kupata sauti rasmi ndani ya Baraza la
Kutunga Sheria la kikoloni, na hivyo kuondoa mfumo wa Kura Tatu kutoka ndani ya
mfumo na walifanikiwa. Kura yako, kwa hiyo, siyo tu hisia bali ni silaha ya
kisiasa inayokuwezesha kuzuia wengine wasiamue mustakabali wako. Kwa kupiga
kura, unazuia wale usiotaka kuongoza wasipate urahisi, na unawaweka madarakani
wale unaoamini wanaweza kutetea masilahi yako.
Kura inalenga
kuleta mazingira ambapo viongozi wanachaguliwa kwa idadi kubwa ya wananchi, na
hivyo wanakuwa na wajibu wa kujibu matakwa ya wapiga kura wao, hasa vijana
ambao ni kundi muhimu la jamii.
"Kiongozi
anayejua amechaguliwa na kura yako lazima akusikilize....Hivyo, kupiga kura ni
kuhakikisha unachagua watu watakaokutetea na kuweka sera zinazokunufaisha."
anasema Mwenyekiti wa Tanzania Bloggters Network Beda msimbe wakati akizungumza
katika kipindi cha radio kilichorushwa na Radio Maria hivi karibuni.
Ndio kusema
kuna wakati katika historia ya Taifa letu kupiga kura haikuwa haki ya kila mmoja,
bali ndoto ya wengi. Leo, kizazi cha vijana kilichozaliwa katika uhuru wa
demokrasia kimerithi fursa adimu fursa ya kuchagua, kuamua, na kushiriki katika
kujenga mustakabali wa Tanzania.
Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa, alitambua mapema kwamba kura ni zaidi
ya karatasi; ni alama ya uhalali wa mamlaka na ishara ya ushiriki wa wananchi
katika uongozi wa nchi yao. Hata katika enzi za chama kimoja, tumeshapata uhuru
Mwalimu Nyerere alisisitiza wananchi wapige kura kama kipimo cha uungwaji mkono,
akiamini kuwa sauti ya wananchi ndiyo msingi wa serikali bora.
“Kura ni
tochi ya kuongoza, inatoa nuru ya uhalali, uwajibikaji, na matumaini,” alisema
Mzee Juma Hiza (78), mwanahistoria na kuongeza: “Tulikipigania hiki
kitambulisho cha kupiga kura. Tuliamini kila raia ana haki ya kusema ‘ndiyo’ au
‘hapana’ kwa amani.”
Mzee hiza
anasema kupiga kura ni tendo la shukrani kwa waasisi wetu.Ni uamuzi wa
kuthamini uhuru uliopatikana kwa jasho, hekima na ujasiri.p na kuwataka vijana
ambao ndio wengi kwenda kuiga kura kwa amani, kwa fahari, na kwa heshima ya
waliotutangulia.
Thamini
mwanga huu, udumishe kwa ushiriki wako.

0 Maoni