WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Oktoba 11, 2025
amepokea kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tuzo ya kutambua mchango
wake katika kusimamia ustawi wa jamii ya watu wenye ulemavu nchini, kwenye
hafla iliyofanyika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Tuzo hiyo imetolewa na taasisi ya Foundation for Disabilities Hope (FDM). Akizungumza kwenye tukio hilo Mheshimiwa Majaliwa amewaeleza kuwa Rais Dkt. Samia yupo tayari kuendelea kufanya makubwa kwa jamii hiyo na ataendelea kuwahudumia.



0 Maoni