Uchaguzi Mkuu
wa 2025 unakaribia, na kwa vijana, huu si wakati wa maneno mengi au siasa za
vijiweni. Ni wakati wa kufanya maamuzi ya kimkakati kwa kuangalia maono
yanayoweza kubadilisha maisha yetu. Kasi, uthubutu na maono — haya ndiyo sasa
yanatakiwa kuongoza kura yako.
Katika
kipindi cha karibu miaka mitano ya uongozi wake, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
ameibuka kama kielelezo cha mafanikio ya Tanzania ya leo, akiongoza taifa kuelekea
kile kinachoweza kuitwa 'Nchi ya Maziwa na Asali' — taifa la fursa, ustawi, na
amani.
Katika
mkutano mkubwa uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Sengerema na Buchosa,
Mkoani Mwanza, Dkt. Samia aliweka wazi dira yake ya miaka mitano ijayo: kujenga
taifa lenye huduma bora, uchumi jumuishi, na maendeleo ya watu wote. Hii ndio
kauli ya kweli ambayo vijana wanatakiwa kuipima.
Mfano wa
Mguso wa Moja kwa Moja:
• Ajira kupitia Kilimo na Uvuvi: Rais
amesisitiza kwamba uchumi wa watu ndio moyo wa taifa. Katika Mwanza, sekta ya
uvuvi imepata mapinduzi makubwa: Serikali imejenga vizimba 400 vya kufugia
samaki, na wavuvi wamewezeshwa kwa boti na mikopo. Mabadiliko haya ni ajenda ya
thamani inayolenga kuongeza kipato na kuchochea biashara moja kwa moja kwa
vijana wanaotegemea sekta hizi.
• Huduma Bora: Ameahidi kuimarisha
afya, elimu, maji safi, nishati, na ajira. Hizi ndizo 'kwa nini' za msingi za
vijana wanapaswa kupiga kura.
Kura Sio
Jazba, Ni Ukomavu wa Kisiasa
Tanzania sasa
ipo katika kipindi cha hamasa ya uchaguzi yenye utulivu. Tofauti na chaguzi za
zamani, dalili zote zinaonyesha kuwa Watanzania wamefikia kiwango kipya cha
uelewa wa kisiasa. Hakuna vurugu, hakuna hofu, bali kuna hamasa ya ushiriki.
Fanya Maamuzi
ya Kimantiki, Si Kihisia
Kwa vijana,
huu ni wakati wa kufanya maamuzi kwa mantiki, si kwa hisia.
Kama unataka:
• Kupunguza gharama za maisha.
• Kupata ajira za moja kwa moja
kupitia miradi mikubwa.
• Kuona miradi inatekelezwa kwa kasi
na ubora.
Basi unapaswa
kupiga kura kwa kiongozi ambaye ameonesha uwezo wa kutafsiri ndoto kuwa matendo
halisi. Kura yako inapaswa kuakisi rekodi ya uthabiti na matokeo, siyo porojo
za kisiasa.

0 Maoni