Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela, MarÃa Corina
Machado, ametangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka huu,
kutokana na juhudi zake zisizochoka katika kupigania haki za kidemokrasia kwa
wananchi wa taifa hilo la Amerika Kusini.
Machado, ambaye amekuwa akiishi mafichoni tangu
uchaguzi wa urais uliofanyika mwaka jana, ametambuliwa kwa "kazi yake ya
kuhamasisha mabadiliko ya haki na yenye amani kutoka utawala wa kiimla kuelekea
demokrasia".
Kamati ya Nobel imeeleza kuwa Machado ni "mmoja
wa mifano ya kipekee ya ujasiri wa kiraia katika Amerika Kusini katika nyakati
za hivi karibuni."
Tangu aanze harakati zake za kisiasa, Machado
amekuwa mstari wa mbele kupinga utawala wa sasa nchini Venezuela, akitaka
mageuzi ya msingi yanayowapa wananchi nafasi ya kuchagua viongozi wao kwa njia
huru na ya haki.

0 Maoni