Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi
akiwahutubia Wananchi waliofika kumsikiliza katika mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Mama Salmini, Mlandizi ndani ya jimbo la
Kibaha Vijijini leo Ijumaa Oktoba 10, 2025 mkoani Pwani.
Katika mkutano huo, Dkt. Nchimbi pamoja na kunadi
Sera na Ilani ya CCM ya 2025-2030,pia alimuombea kura za ushindi wa kishindo
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani.
Pamoja na mambo mengine,Dkt Nchimbi pia alitumia
nafasi hiyo kuwanadi wagombea Ubunge wa
mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Kibaha Mjini Ndugu Silyvestry
Francis KOKA, mgombea Ubunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Ndugu Hamoud Abuu
JUMAA pamoja na Madiwani.



0 Maoni