MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amewahutubia Wananchi kwenye mkutano mdogo wa hadhara uliofanyika
katika uwanja wa CCM, Kata ya Sanya Juu ndani ya jimbo la Siha, Wilayani
Siha,akiendelea na mikutano yake ya Kampeni
leo Jumamosi Septemba 13,2025 mkoani Kilimanjaro.
Baada ya kuwasalimia Wananchi hao, Dkt Nchimbi ambae ni
mgombea mwenza wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,pia alitumia nafasi hiyo
kuwanadi Wagombea Ubunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Siha
Ndugu Godfrey Mollel pamoja na Madiwani.
Dkt.Nchimbi ambae ameingia Kanda ya Kaskazini,akianzia
mikutano yake ya Kampeni Mkoani Arusha na
sasa ameingia mkoa wa Kilimanjaro kusaka kura za ushindi wa Kishindo za
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi
Mkuu ya mwaka 2025-2030, ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya
wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.
Ngombea mwenza huyo amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.
0 Maoni