MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel
John Nchimbi, amewasili Wilaya ya Same
kuwahutubia Wananchi wa jimbo la Same Magharibi kwenye mkutano wake mdogo,leo
Jumapili Septemba 14,2025 mkoani Kilimanjaro.
Dkt.Nchimbi ambae ni mgombea mwenza wa Rais Dkt.Samia Suluhu
Hassan anaendelea na Mikutano yake ya kampeni mkoani Kilimanjaro,sambamba na
kuwanadi Wagombea Ubunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Same Magharibi,Ndugu
Dkt.Mathayo David Mathayo pamoja na Madiwani.
Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi
Mkuu ya mwaka 2025-2030, ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya
wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.
Ngombea mwenza huyo amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.
0 Maoni