Watoto wapo hatarini zaidi kutokana na uchafuzi wa hewa

 

Wataalamu wa afya wameshauri kuchukuliwa kwa hatua za haraka na madhubuti ili kupunguza kiwango cha uchafuzi wa hewa, huku wakisisitiza umuhimu wa sera za mazingira zinazolenga kulinda afya ya wananchi hasa watoto. 

Wataalamu wameonya kuwa uchafuzi wa hewa umefikia viwango vya hatari na sasa unatishia siyo tu afya ya mapafu bali pia unasababisha kiharusi, magonjwa ya moyo, matatizo ya akili ya kusahau (dementia), wasiwasi na msongo wa mawazo (depression). 

Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO), watu tisa kati ya kumi duniani wanapumua hewa chafu isiyokidhi viwango salama vya kiafya. Uchafuzi huo unajumuisha chembe chembe ndogo ambazo zinaweza kuingia ndani kabisa ya mapafu na hata kufikia ubongo wa binadamu.

Chapisha Maoni

0 Maoni