Sheria haziendi likizo wakati wa uchaguzi - Dkt. Ndumbaro

 

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, ameitaka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) kuongeza umakini katika kutekeleza majukumu yake kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu, akisisitiza kuwa sheria haziendi likizo kipindi cha uchaguzi.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 16 kwa ofisi za mashtaka za wilaya 16, Dkt. Ndumbaro amesema uzoefu unaonyesha kuwa katika kipindi cha uchaguzi baadhi ya watu hufanya vitendo vinavyotishia amani, jinai, kashfa na udhalilishaji wakiamini sheria hazifanyi kazi.

Waziri Dkt. Ndumbaro ameongeza kwa kutaka kila anayekiuka sheria achukuliwe hatua bila kujali nafasi yake, “Machafuko mengi yanatokea kipindi cha uchaguzi, msimfumbie macho watu wanaovunja sheria.”

Chapisha Maoni

0 Maoni