Wageni mbalimbali wanaendelea kumiminika kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba wakijionea fursa zinazotolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii, hususan kwenye sekta ya misitu na utalii wa ikolojia.
Miongoni mwa wageni hao
ni Mwana wa Mfalme Celipilo Ngobese kutoka Kwazulu Natal, Afrika Kusini, ambaye
leo Julai 11, 2025 ametembelea banda la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(TFS).
Ngobese alipata fursa ya
kuona shughuli za ufugaji nyuki, uhifadhi wa misitu na vivutio vya utalii wa
ikolojia vinavyosimamiwa na TFS, akieleza kuvutiwa na jitihada za Tanzania
katika kuhifadhi rasilimali za misitu na kuzitumia kwa maendeleo endelevu.
Maonesho ya SabaSaba
yanaendelea Jijini Dar es Salaam yakihusisha taasisi mbalimbali za serikali na
sekta binafsi, huku yakilenga kuvutia wawekezaji na wadau wa
ndani na nje ya nchi.




0 Maoni